Matokeo ya Azam vs KCCA ya Uganda yasikupite mtu wangu!!

Klabu ya Azam imeanza vyema michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam baada ya kuwafunga KCCA ya Uganda bao 1-0.
John Boko ndiye aliyeiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika kipindi cha kwanza dakika ya 12 akipokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.
Yanga ilianza vibaya michuano hiyo jana baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved