Benki kuu Tanzania imejibu kwanini sarafu mpya ya shilingi 500 haipo sana kwenye mzunguko

Kwenye hii post tumeipata benki kuu ya Tanzania ambayo iko tayari kuzungumzia ishu ya sarafu mpya ya shilingi mia tano kutoonekana sana kwenye mzunguko wa fedha nchini Tanzania.
‘Benki kuu iliamua kubadilisha kutoka noti na kuleta sarafu ya shilingi mia tano baada ya kuona noti hiyo inakuwemo kwenye mzunguko kwa muda mrefu kuliko inavyotakiwa bila kurudishwa Benki hivyo inachakaa mno’
 ‘Katika zoezi hilo la kuibadilisha noti ya shilingi mia tano kuwa sarafu, utakuta kwamba Benki kuu sehemu sehemu ambayo inaanza usambazaji ni kwamba wanatoa pesa kwa benki za biashara na zinapokuja huwa tunawatolea wachukue sarafu na noti lakini kwenye kipindi hiki benki hizi zimekua hazichukui sana sarafu ya shilingi mia tano kama zinavyochukua noti, ila sarafu hii ipo kabisa‘

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved