POLISI WATANGAZA ZAWADI YA MILLION 50 KWA YEYOTE ATAKAYEFANIKISHA HILI

 
Jeshi la polisi Tanzania limetangaza kutoa zawadi nono ya shilingi za kitanzania million 50 kwa mtu yeyete mwenye taarifa za uhakika na za haraka zitakazofanikisha kuwakamata wote waliovamia kituo cha polisi stakishari na kuua askari na raia waliokuwa katika kituo hicho usiku wa kuamkia jana.
Akitoa Taarifa mbele ya wanahabari leo kamishna wa polisi kanda maalum ya dare s ealaam SULEMAN KOVA  amesema kuwa kupitia dhana ya polisi ya ulinzi shirikishi mkuu wa jeshi la polisi IGP ERNEST MANGU ameona ni muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika suala hili linalohusiana na ulinzi na usalama wao na watanzania wote kwa ujumla. 
Mtu yeyote atakaye jishughulisha na hili kwa kutoa Taarifa sahihi atoe Taarifa kwa vioongozi wakuu wa jeshi la polisi waliopo karibu au apige namba zifuatazo---

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM (CPS.H KOVA) -----0754034224
MSEMAJI WA JUESHI LA POLISI (SSP ADVERA BULIMBA)-----0713631667
MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI (CP DIWANI ATHMAN)----0715323444

Aidha wananchi wenye taarifa husika pia wanaweza kuonana uso kwa uso na viongozi wakuu wa makao makuu ya polisi au kanda maalum na kuwapa taarifa moja kwa moja
Kamishna kova amesema kuwa mwananchi ambaye ataleta taarifa husika na kufanikisha zoezi hilo itafanyika siri kubwa na hatajulikana popote kama yeye ndiye mtoa taarifa husika

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved