Habari kutoka kwa chanzo zimeeleza
kwamba, hivi karibuni, Rose alilipwa Sh. milioni 3 kwa ajili ya shoo
huko Makambako mkoani Njombe na matangazo yakafanyika lakini hakutokea.
Ikadaiwa kuwa, wakati matangazo ya shoo
yakiendelea, mtu mwingine aliyekuwa akimdai Sh. milioni 3.5 (pia
alichukua fedha kwa shoo siku za nyuma) alikwenda Makambako kwa lengo la
kumsubiri Rose ili amnase, lakini hakutokea.
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga
‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao waliripoti ishu ya Rose, Kituo cha Polisi
Makambako ambapo polisi walifunga safari kumfuata Dodoma.
Sosi huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa
Juni 27, mwaka huu na kuswekwa rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma
tayari kwa kupelekwa mahakamani. Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali
mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na
kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu
anamsimamia kazi zake.
“Msama alikubali kwa sharti kwamba, kwa
sababu ana kazi ya kufanya na Rose hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie,
yeye na Rose watakatana kwenye kazi.
“Rose alisafirishwa Juni 29, mwaka huu
akiwa chini ya ulinzi wa askari wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala
naye chumba kimoja hotelini. Kesho yake wakaenda ofisini kwa Msama,
Block 41, Kinondoni, akalipa milioni sita na laki tano keshi,” kilisema
chanzo.
Baada ya kunyetishiwa skendo hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Msama ambapo alidai waulizwe wafanyakazi wake.
Mmoja wa wafanyakazi wake aliyeomba hifadhi ya jina, alikiri Msama kumlipia Rose kiasi hicho cha pesa.
Mmoja wa wafanyakazi wake aliyeomba hifadhi ya jina, alikiri Msama kumlipia Rose kiasi hicho cha pesa.
“Ni kweli! Rose aliletwa hapa toka
Dodoma chini ya ulinzi wa polisi wawili. Msama akamlipia shilingi
6,500,000 ambazo watakatana kwenye kazi zao,” alisema mfanyakazi
huyo.Rose alipotafutwa, Alhamisi na Ijumaa iliyopita, simu yake ilikuwa
ikiita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment