MSHAMBULIAJI nyota wa Uganda, Emmanuel Okwi ana nafasi nzuri ya kuula
endapo atafanikiwa kufanya vizuri katika majaribio nchini Denmark mwezi
huu.
Okwi anayechezea Simba, anatarajiwa kwenda nchini Denmark kufanya
majaribio katika Klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu ya huko
kuanzia kesho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya Klabu ya Simba
jana, majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia kesho na baada ya hapo
klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio hayo.
Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Simba inafurahi sana kuona
wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye
viwango vya kimataifa zaidi, hivyo Simba inamtakia kila la kheri Okwi
kwenye majaribio yake ya siku 14 kwenye Klabu ya Sonderjyske iliyopo
kwenye ligi ya Denmark.”
Okwi aliyezaliwa miaka 23 iliyopita nchini Uganda, aliwahi pia
kucheza kwa muda mfupi katika Klabu ya Etoile Sportive du Sahel ya
Tunisia na baadaye kuichezea Yanga kabla ya msimu uliopita kurudi klabu
yake ya Simba.
Katika hatua nyingine, mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco
mambo yake yamemnyookea baada ya Klabu ya Free State Stars ya Afrika
Kusini kukubali kumsajili.
Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari, Azam FC
imekubali kumuuza mchezaji huyo na kinachosubiriwa ni timu hiyo
kumalizana juu ya maslahi binafsi ili kuhamia katika timu hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa bongostaz, Azam FC imekubali kumuuza
mshambuliaji huyo kwa kitita cha Dola za Marekani 80,000 ikiwa ni sawa
na zaidi ya Sh milioni 160,000 kwa klabu hiyo.
Na sasa kinachosubiriwa na Free State kumalizana na mchezaji juu ya
maslahi binafsi ili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, ahamie
Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
Mshambuliaji mahiri, Mrisho Ngassa aliyesajiliwa na Free State miezi
miwili iliyopita baada ya kumaliza mkataba Yanga, anaeleza kuwa ndiye
aliyempa ulaji huo Bocco kwa kuwapa viongozi wa timu hiyo mawasiliano ya
Bocco.
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd
kuzungumzia taarifa hizo, alisema hazina ukweli na kama zitakuwa na
ukweli zitawekwa mara moja katika tovuti ya klabu hiyo.
Bocco aliwahi kufanya majaribio Afrika Kusini katika Klabu ya Supersport na Algeria na kufuzu ila hakuuzwa kutokana na dau dogo
No comments:
Post a Comment