Serikali ya Kenya yatangaza vita vikali dhidi ya ushoga
Makamu wa Rais wa Kenya amesisitiza kuwa, serikali ya nchi hiyo haiwezi
kuvumilia hata kitengo vitendo vya maingiliano ya watu wa jinsia moja.
Msimamo huo wa William Ruto umekuja siku chache tu kabla ya kuwasilia
Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya. Matamshi hayo ya Makamu wa
Rais wa Kenya yamekuja kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo
iliyodai kuwa watu wanaotenda vitendo hivyo vichafu wana haki ya kuwa na
chama chao. William Ruto amenukuliwa na vyombo vya habari akisema
jijini Nairobi leo Jumapili kwamba, maingiliano ya watu wa jinsia moja
ni kinyume na maumbile ya Mwenyezi Mungu. Amesema, Mwenyezi Mungu
hakumuumba mwanamme ili aolewe na mwanamme mwenzake wala mwanamke ili
aolewe na mwanamke mwenzake. Amesema: "Tumesikia kuwa Marekani
wanaruhusu ushoga na vitendo vingine vichafu. Ninapenda kusema nikiwa
kiongozi Mkristo kwamba tutailinda nchi yetu ya Kenya na tutasimama
imara kulinda imani yetu ya kidini na kulinda nchi yetu." Makamu wa Rais
wa Kenya pia amewataka Waislamu na Wakristo kuunganisha nguvu zao na
kusimama kidete kulinda imani zao mbele ya jaribio lolote la kutaka
kuruhusu vyama vya mashoga nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment