Mahakama ya Misri imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 10 jela dhidi ya
wanaharakati 25 wa nchi hiyo kwa madai ya kushiriki katika fujo
zilizozuka baada ya jeshi kumpindua Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo.
Mbali
na kifungo jela, Jaji Mootaz Khaffaji, mkuu wa mahakama ya makosa ya
jinai ya al Jizah ametoa adhabu ya kulipa karibu Pound 275 (karibu dola
35 elfu za Kimarekani) dhidi ya watuhumiwa hao kama fidia ya hasara
walizosababisha wakati wa machafuko hayo.
Tarehe pili Augosti 2013,
kulizuka machafuko baina ya wafuasi wa Mohammad Morsi na jeshi la polisi
la Misri yaliyosababisha hasara za mali na roho za watu.
Wakati huo
huo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri leo Jumapili imetangaza kuwa,
vikosi vya nchi hiyo vimewatia mbaroni wanachama 52 wa Ikhwanul Muslimin
ikiwa ni katika operesheni za vikosi hivyo vya kuchukua hatua za
kiusalama. Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, wanachama hao wa
Ikhwanul Muslimin wanatuhumiwa kuhusika katika mashambulizi dhidi ya
maeneo ya uma na binafsi na kuchochea watu kupinga serikali katika mikoa
tofauti ya Misri.
No comments:
Post a Comment