Daesh yauza kimagendo vitu inavyoiba Syria na Iraq
Wataalamu wa athari za kale na wataalamu wa vitendo vya uhalifu wamesema
kuwa athari za kale zinavyoibiwa na kundi la kigaidi na kitakfiri la
Daesh zinauzwa kimagendo nchini Unigereza. Wataalamu hao wamesema kuwa,
tofauti na linavyodai kundi la kitakfiri la Daesh kwamba linavunja
athari za kale huko Syria na Iraq kwa sababu ni nembo za shirki, uhakika
wa mambo ni kuwa, genge hilo la kigaidi linapora athari za kale za nchi
hizo mbili na kuziuza kimagendo katika nchi za Ulaya kama njia ya
kujipatia fedha. Gazeti la The Guardian la nchini Uingereza limeripoti
kuwa, athari hizo za kale ni pamoja na vyombo vya udongo, vioo vya kale,
visanamu vidogo na kazi nyingine za kale zenye thamani ya mamia ya
maelfu ya dola. Hii ni katika hali ambayo Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO wiki iliyopita lilielezea wasiwasi
wake kuhusu suala hilo na kusema kuwa kundi la kigaidi la Daesh linaiba
kiwango kikubwa cha athari za kihistoria za Iraq na Syria. Mkurugenzi
mkuu wa shirika hilo alisema mjini London Uingereza kuwa kundi la
kigaidi la Daesh linauza athari za kale za kihistoria za Iraq na Syria
kwa madalali na kujiingizia fedha nyingi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment