Mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 yanaendelea huko
Vienna, Austria kwa lengo la kutatua hitilafu zilizosalia kabla ya
kutiwa saini makubaliano ya mwisho kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran.
Habari
zinasema kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Marekani, Muhammad
Jawad Zarid na John Kerry wamekutana na kufanya mazungumzo leo mjini
Vienna huku Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran, Dakra Ali Akbar Salehi
akikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Marekani, Ernest
Moniz.
Sambamba na hayo manaibu mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na
kundi la 5+1 pia pamoja na wataalamu wanaendelea kufanya mazungumzo ya
dakika za mwisho yanayolenga kumaliza hitilafu zilizosalia kati ya pande
hizo mbili hususa suala la jinsi ya kufutwa vikwazo dhidi ya Iran.
Ilitazamiwa
pia kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza
wangejiunga na mazungumzo hii leo Jumapili huko Vienna. Mawaziri wa
Mambo ya Nje wa Russia na China wanatazamiwa kuwasili Vienna kesho, siku
moja kabla ya siku ya mwisho iliyoainishwa kwa ajili ya kufikia
mapatano kamili ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1.
No comments:
Post a Comment