Wamarekani washerehekea uhuru wa miaka 239

Rais wa Marekani ametuma salamu za pongezi kwa wamarekani wote katika hotuba yake ya kila wiki. Siku hiyo pia inaadhimisha miaka 17 ya kuzaliwa mtoto wake mkubwa Malia.
Kote Marekani Jumamosi Julai 4 wananchi wanasherehea miaka 239 ya uhuru wa nchi yao kutoka kwa mkoloni mwingereza , huku maafisa wa usalama wakizidi kuimarisha ulinzi na usalama kufuatia tishio la uwezekano wa ugaidi kufanyika katika suikukuu ya julai 4.
Rais wa Marekani ametuma salamu za pongezi kwa wamarekani wote katika hotuba yako ya kila wiki. Siku hiyo pia inaadhimisha miaka 17 ya kuzaliwa mtoto wake mkubwa Malia.
Familia ya rais Obama itaadhimisha siku hii kwa kufanya “ nyama choma”  katika uwanja wa ikulu ya white house, kwa ajili ya maafisa kadhaa wa jeshi na familia zao.
Nje ya Washington , mkurugenzi wa CIA John Brennan alizungumza katika sherehe za kuapishwa raia wapya 100 wa marekani huko Mount Vernon,  Virginia.
Maelfu ya wamarekani wamemiminika katika jiji kuu la Marekani , Washington kushuhudia matamasha mbalimbali yatakayotumbuliza katika Mall ya taifa usiku wa Jumamosi.
Matamasha hayo yatajumuisha wasanii Barry Mnillow, Alabama, KC, na Sunshine Band, Nicole schrizinger na wengine wengine.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved