Wananchi 32 wa Yemen wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika
siku ya mia moja ya mashambulio ya kikatili ya Saudi Arabia dhidi ya
nchi hiyo ya Kiarabu.
Ndege za kijeshi za Saudia mapema leo Jumamosi zimefanya mashambulio kadhaa kwenye maeneo tofauti ya Sana'a, mji mkuu wa Yemen.
Mtandao
wa habari wa Sabanet umeripoti leo kuwa, raia 10 wa Yemen wameuawa na
wengine wengi kujeruhiwa baada ya ndege za Saudia kushambulia makazi ya
raia kwenye eneo la Baytul Faqih katika mkoa wa al Hudaydah, magharibi
mwa Yemen.
Raia wengine wanne wa Yemen wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa baada ya ndege za adui kushambulia eneo la Jaraf mkoani Sana'a.
Raia
wengine watatu wa Yemen wa familia moja wameuawa na wengine kadhaa
kujeruhiwa katika mashambulizi ya Saudia kwenye eneo la an Nahdha huko
Sana'a.
Saudia Arabia inaendeleza mashambulizi yake ya kikatili dhidi
ya wananchi wa Yemen bila ya kujali kuwa wananchi hao Waislamu wamo
katika funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment