Kwa kawaida tumezoea kuona watoto wenye
umri wa miaka 15 kuwaona wakiwa elimu ya sekondari hii, imekuwa tofauti
kwa mtoto huyu kutoka Thulamahashe Mpumalanga Afrika Kusini kujiunga na chuo cha medicine nchini humo. Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Decent Junior Mkhombo amejiunga na wanafunzi wenzake kwenye chuo hiko kilichofunguliwa mwaka huu nchini Afrika Kusini kwa lengo la kusomea medicine katika chuo hiko cha University of Limpopo (UL).
Serikali nchini humo imetenga zaidi ya
billion 1.3 kwa ajili ya masomo ya wanafunzi wote wanaotarajiwa
kujiunga na chuo hiko, ambao baadae watasaidia matatizo ya afya nchini
humo. Decent Junior Mkhombo amekuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo nchini humo kusomea udaktari lakini mwaka 2014 Dr.Sandile Kubheka alikuwa mwanafunzi wa kwanza kufuzu mafunzo ya udaktari nchini humo akiwa na umri wa miaka 21
“Nina
mapenzi ya kujifunza oncology kwa sababu kansa ni ugonjwa mkubwa sana
na unatakiwa kupatiwa tiba, kikukweli hatuna maktaba, tuna mahabara kwa
jina lakini haina vitendea kazi vya kukidhi, lakini tuna waalimu wazuri
kama Mr Richard Walusimbi ambaye amekuwa akitaka tujitume siku zote”
>>> Mkhombo
No comments:
Post a Comment