Watu
sita wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika
pori la akiba la Maswa.
Kukamatwa
kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John Magufuli, kutoa
agizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa waliohusika na tukio
hilo na kufikishwa katika mkono ya sheria.
Kauli
hiyo ya Rais iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu,
Gerson Msigwa, ilisema Rais Magufuli mbali na kusikitishwa na tukio
hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha inaendeleza
mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zote na kuwataka wananchi na wadau
mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana alithibitisha kukamatwa kwa watu hao.
Alisema awali walikamata watu wawili, juzi watatu na jana mmoja wote wakiwa wakazi wa Simiyu na uchunguzi bado unaendelea.
Ijumaa
iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo wakati
ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba majangili
walikuwa wameua tembo mmoja.
Katika
tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower
(37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.
No comments:
Post a Comment