Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu tangazo la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuwa kesho wamepanga kufanya maandamano hadi Ikulu kwa lengo la kuishinikiza serikali kubadili msimamo wake kuhusu TBC kutorusha Live baadhi ya vikao vya Bunge.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amepiga marufuku
maandamano hayo na kuwataka vijana hao kutumia njia mbadala za kupata
ufumbuzi wa suala hilo badala ya maandamano.
Akitoa
sababu za kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, Kamanda Sirro alisema
kuwa hakuna taarifa na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo
yatapokewa na Rais Magufuli.
Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo.
“Siku
hiyo sio nzuri sana kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni
siku ambayo wengi watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za
kijamii. Na kwa sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu
hiyo, nisema tu kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.
No comments:
Post a Comment