WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua
Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias
Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.
Kabla
ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo
Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016.
Chanzo Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment