Bungeni: Mbunge Magdalena Sakaya Aituhumu Serikali Kuwa Chanzo Cha Ukosefu Wa Ajira Kwa Vijana

Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora Magdalena Sakaya CUF amesema tatizo kubwa la ajira nchi hii linachangiwa na serikali yenyewe.

Magdalena ameyasema hayo wakati akichangia mpango wa serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambao uliwasilishwa hapo juzi na wabunge kupewa nafasi ya kuchangia na kuishauri serikali kwa muda wa siku 5.

"Mheshimiwa Naibu Spika nchi hii ni tajiri sana tuna misitu ya kutosha lakini cha kushangaza tunakata miti tunasafirisha kwenda nje kwenda kutengeneza vifaa ambavyo tunakuja kuuziwa kwa bei ya juu wakati vijana nchini hawana ajira wanarandaranda mitaani". Alisema Sakaya na kuomngeza;

"Serikali ndiyo chanzo cha kukosekana kwa ajira kwa vijana nchi hii maana hadi pamba za kusafisha masikio tunatoa nje, pia tumeifanya nchi hii kuwa nchi ya kupokea kila kitu wakati malighafi tunazalisha hapa hapa nchini,Serikali ifufue viwanda ili kuweza kuajiri maelfu ya vijana".

Aidha Mbunge huyo ameitaka serikali kutekeleza kwa vitendo miradi ya maji ambayo iliahidiwa katika wilaya ya Kaliua na kwa muda wote wa mpango uliopita vijiji vitatu tuu ndivyo viliweza kupewa kipaumbele.
Chanzo cha habari Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved