Serikali
imekiri kuwepo kasoro nyingi zilizojitokeza katika mradi Mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ikiwamo ubadhirifu wa
fedha kwa Kaya sizizokuwa na sifa kupewa pesa kupitia mpango huo hivyo
imejipanga kuborsha zaidi mpango huo katika awamu ya tatu kwa
kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa.
Akijibu
swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza
ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na
kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa
kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka
Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka
vigezo vya Kaya maskini.
“
Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi
kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo
zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna
malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya
nyingine ambazo sio maskini
"Kwa
kuliona tatizo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu
watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya
zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya
yoyote atakaye bainika kufanya hivyo
“Mpaka
sasa kutokana na malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya
maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewawajibisha watendaji
toka Wilaya za Karagwe, Kagera , kibondo na Kigoma na tuomba kupewa
taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na
tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia
watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.
Aidha
Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa
fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa
hizo sio za kweli kwani fedha hizi zinatolewa na Serikali ili kusaidia
Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu
Malazi na chakula bora.
TASAF
ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka
hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment