WATANZANIA wameshauriwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea
maendeleo badala ya kukaa vijiweni na kuwajadili watu, jambo ambalo
haliwezi kuwapa tija yoyote.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
wakati alipofika mjini Bukoba kwa lengo la kutafuta wadhamini, ikiwa ni
hatua mojawapo ya kutekeleza utaratibu wa CCM kwa makada wake wanaowania
uongozi katika nafasi mbalimbali.
Kwa upande wa Urais, nafasi anayoiomba Lowassa sambamba na makada
wengine zaidi ya 30, sharti mojawapo ni mgombea kuwa na wadhamini 450
kutoka jumla ya mikoa 15 Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema wakati umefika watu waanze kubadili mawazo ya kutoka katika
hali ya kukaa vijiweni na kupita wakiwakejeli wenzao kwa maneno
yasiyofaa bali watumie muda mwingi katika kufanya kazi ili waweze
kujiletea maendeleo endelevu yatakayowafanya waishi bila kulalamika.
Lowasa katika mkoa wa Kagera amepata wadhamini 6,500.
No comments:
Post a Comment