MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambaye pia
ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda ameanza
safari ya kusaka wadhamini kwa kuzuru Mkoa wa Katavi.
Pinda aliyewasili Mpanda juzi jioni, alipokewa na maelfu ya wakazi wa
mji wa Mpanda ambao waliamua kumsindikiza kwa mchakachaka na bodaboda
kutoka uwanja wa ndege hadi nyumbani kwake, Makanyagio.
Kufikia jana mchana alikuwa amekwishapata wadhamini 4,243 kwa kuzuru vituo viwili tu vya Inyonga na Mpanda Mjini.
Ratiba yake inaonesha atazuru vituo vitatu katika mkoa wa Katavi.
Katika kituo chake cha kwanza, aliwasili Inyonga yalipo makao makuu ya
wilaya yake ya Mlele ambako alipata wadhamini 1,440.
Alirejea Mpanda saa 9 mchana ambako katika ofisi ya CCM Wilaya alipata wadhamini 2,803.
Hata hivyo, bado anaendelea na safari ya kuelekea kijijini kwake
Kibaoni, kata ya Mpimbwe, wilayani Mlele ambako ni upande wa bondeni wa
wilaya ya Mlele ambako pia alikuwa anasubiriwa na wadhamini wake.
No comments:
Post a Comment