Fetty Da Santos:Sina tabia ya kutoka na Ma'producer'..

Fetty Da Santos
Yule mtangazaji maarufu ndani ya Mbeya na Nyanda za juu kusini,Fetty Da Santos,siku ya jana amefunguka ndani ya NDT kuhusu uzushi kumuhusu yeye na kusema kuwa yeye hana kawaida ya kutembea na ma'producer',bali aliwahi kuwa na uhusiano na Producer mmoja wa muziki aitwaye Van Cigger,na baada ya hapo hadi sasa yuko na 'songwritter','singer' na 'director' G-Sacha.
Pia Fetty aliweka bayana swala la kutojihusisha kimapenzi na mtangazaji mwenzake Chris Bee,bali ni shemeji yake wa nguvu,akisema "Chris B ni kaka wa G-Sacha, so muda mwingine nakuwa naye wakati siko na G,si unajua mume analinda jiko lake?"
Fetty ameongelea pia sababu ya kuhama kutoka Sweet Fm na kwenda Mbeya Highlands Fm,akisema "Niliondoka Sweet Fm kwa sababu za kimaslahi na siyo ugomvi wowote,kama unavyojua watangazaji sasa ni kama wachezaji wa mpira,tunafuata kwenye malipo bora zaidi".
Fetty Da Santos pia alimbia NDT kuwa tayari ameshiriki katika filamu moja ambayo bado haijatoka,na ana mpango wa kushiriki filamu zingine pia akihitajika.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved