Mafuta kuanza kushushwa bandari ya Tanga

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
MAFUTA yataanza kushushwa katika Bandari ya Tanga kuanzia Julai mwaka huu katika mpango unaolenga kuondoa utegemezi wa Bandari ya Dar es Salaam pekee.
Aidha,mpango huo utaimarisha upatikanaji wa bidhaa za petroli nchini na kupunguzamsongamano katika Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji,imeelezwa.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Pichani) aliliambia Bunge juzi kuwa serikaliinafanya tathmini ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari ya Tangaili sehemu ya shehena ya mafuta kupitia Mfumo wa Uagizaji wa Mafutakwa Pamoja(BPS) yaweze kushushwa kwenye bandari hiyo.
“Tunategemeakazi hii itaanza Julai mwaka huu na hatua hii itaisaidia kuimarisha uchumi waMkoa wa Tanga,” alisema. Simbachawene alipowasilisha bajeti ya wizara yake kwamwaka wa fedha 2015/2016.
Aidha,alisema mwaka 2015/16, serikali itaendelea kuboresha shughuli za udhibiti wabidhaa za petroli na Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja nchini ikiwemokubadilisha muundo wa kampuni inayosimamia uagizaji huo wa pamoja (PICL).
Aidha,alisema katika mwaka 2014/15, serikali ilikamilisha maandalizi ya Kanuni zaUratibu wa Hifadhi ya Taifa ya Mafuta. “Serikali kupitia TPDC pia imekamilisha majadiliano na Kampuni ya Oman TradingInternational (OTI) kwa ajili ya kuiuzia TPDC mafuta atakayotumika kwenyeHifadhi ya Taifa ya Mafuta,” alisema Simbachawene.
“Aidha,Ewura inakamilisha maandalizi ya Kanuni zitakazotumika kukokotoa bei ya mafutakutoka kwenye Hifadhi ya Taifa. Baada ya kukamilisha taratibu zote, uendeshajiwa hifadhi hiyo utaanza mwaka 2015/16.” Kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Waziri alisema imeandaa Kanuni kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini.
“Aidha, ilikuboresha usambazaji wa bidhaa za petroli hapa nchini, Ewura inaendelea natathimini ya kuanzisha mfumo mpya wa usambazaji mafuta kwa kutumia magari navituo vidogo vinavyohamishika,” alisema.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved