Mkapa kuzindua filamu ya DCB

RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya mpya ya Kiswahili iliyopewa jina la ‘Hamu ya Mafanikio’ ambayo ina maudhui ya kutoa elimu na kuhamasisha wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kutumia huduma za kibenki, ambazo zinabadilisha maisha.
Filamu hiyo ambayo imetayarishwa kwa ushirikiano baina ya Benki ya Biashara ya DCB na kampuni ya Concert Group, imepangwa kuzinduliwa Juni 25 mwaka huu katika ukumbi wa Century Cinemax jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es salaam jana Meneja Mkuu wa wateja wadogo na wakubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku alisema kuwa, DCB imeamua kuandaa filamu hiyo baada ya kutambua kuwa watanzania wengi wanapenda kuangalia filamu za Kiswahili na hivyo anaamini wataweza kuwafikia watu wengi zaidi.
“DCB Bank tumeona njia pekee ya kuwafikia Watanzania walio wengi ni kupitia sanaa, na sana kupitia filamu imeonekana kupendwa zaidi na watu wengi hivyo tutatoa elimu juu ya huduma zetu za kibenki, lakini pia jamii itapata burudani,” alisema Machaku.
Filamu hiyo ya Hamu ya Mafanikio imewashirikisha wakali mbalimbali wa filamu nchini akiwepo Tito Zimbwe, Rose Ndauka, Jackline Pentezel, Abdul Mhema, Hidaya Njaidi, Gojah na wasanii wengine mbalimbali.
Mchaku alisema baada ya kuzinduliwa kwa filamu hiyo, itaoneshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, hasa katika matawi ya benki hiyo na katika uzinduzi huo filamu hizo zitapatikana na zitakuwa zikiuzwa kwa gharama nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii walioshiriki katika utengenezaji wa filamu hiyo, Ndauka alisema itamjenga sana mwananchi atakae iangalia na kumpa ujasiri na uwezo wa kutumia huduma za kibenki DCB.
“Ndani ya filamu utaona jinsi kijana Jensen ambaye aliweza kupata elimu yake hata baada ya kufiwa na wazazi wake ambao walimfungulia akaunti ya wanafunzi na pia kijana huyo kupitia akaunti ya biashara ilimwezesha kufanya biashara kwa kupata mikopo mbalimbali,” alisema Ndauka.
Filamu hiyo inakuja wakati benki nyingi zikikabiliwa na changamoto ya jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved