Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza kuhusu hali mbaya
inayowakabili wagonjwa wa saratani nchini humo.Wizara ya Afya ya Yemen
leo imetangaza kuwa kituo cha afya kinachowahudumia wagonjwa wa saratani
huko Sana'a mji mkuu wa nchi hiyo kinakabiliwa na upungufu wa dawa
kutokana na mashambulizi ya Saudia yanayoendelea kila uchao, huku
wagonjwa wakiwa na hali mbaya. Wizara ya Afya ya Yemen imeongeza kuwa
kituo hicho kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa dawa za wagonjwa wa
saratani kutokana na kuzingirwa Yemen na kwamba hali hiyo imewaathiri
pakubwa wagonjwa ambao wametokea katika mikoa ya karibu na Sana'a na
kuja katika kituo hicho wakiwa na matarajio ya kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment