Human Rights Watch yalaani jinai za Saudia Yemen
Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limelaani jinai
zinazoendelea kufanywa na Saudi Arabia za kuua raia wasio na hatia huko
Yemen na kutaka uchunguzi ufanyike na kufidiwa hasara zote
zilizosababishwa na Saudia katika mashambulizi yake ya kikatili kwenye
nchi hiyo ya Kiarabu. Mtandao wa habari wa Sabanet umenukuu ripoti ya
shirika hilo yenye kichwa cha maneno "Mashambulizi Yaliyo Kinyume cha
Sheria ya Saudia Nchini Yemen" na kuongeza kuwa, ndege za Saudi Arabia
tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili 2015 zimekuwa zikivunja sheria zote za
kivita kwa kushambulia maeneo ya raia huko Saada Yemen na kuharibu nyuma
za makazi ya watu pamoja na masoko na shule kadhaa vikiwemo pia vituo
vya mafuta. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, makumi ya raia wa Yemen wameuawa
kwenye mashambulio hayo wengi wao wakiwa ni watoto wadogo. Bi Sarah
Leah Whitson, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki za Binadamu la
Human Rights Watch katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa
Afrika amesema kuwa, mashambulio ya ndege hizo za Saudia yanavunja
sheria za kivita na inabidi uchunguzi kamili ufanyike kuhusu jinai hizo.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia kijeshi Yemen tangu tarehe 26 Machi,
na hadi sasa maelfu ya watu wameshauawa na kujeruhiwa kwenye jinai hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment