Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco akishangilia goli lake
Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The
Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017
nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.
Stars
ambayo imeonekana kabadilika ikicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka
mwisho wa mchezo na hali hiyo iliyowaduwaza wenyeji Uganda.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Rashid Mandawa (kushoto) akijaribu kumtoka Hassan Waswa
Mpaka
dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 - 0
Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi
mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John Bocco na Rashid Mandawa.
Dakika ya
58, John Bocco aliipatia Tanzania bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira ndani ya eneo la
hatari.
Baadhi ya Watanzania waliokwenda Uganda kuipa sapoti Stars
Mara
baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa
Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 82, kupitia kwa
mchezaji Kizito Hezron.
Mpaka
dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo
Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa
watakutana na Sudan.
Kikosi cha Stars kilichoanza dhidi ya Uganda
Mara
baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema
anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri,
timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja
iliyopatikana.
Mkwasa
amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti kwani wamekaa na kwa wiki
moja tu lakini imeonesha mabadiliko , hivyo wanahitaji muda mrefu kukaa
na vijana ili kujenga timu bora.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa
Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin
Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John
Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
No comments:
Post a Comment